Cardi B awasapraizi mashabiki wake
Muktasari:
- Huyo ni mtoto wa kwanza kwa wawili hao na Cardi B alichapisha picha zilizoleta hisia kali kupitia akaunti ya Instagram, ikionyesha kichanga hicho kikiwa mikononi mwake kwa upendo.
RAPA mwenye tuzo ya Grammy, Cardi B amewafanyia sapraizi mashabiki wake duniani kwa kuianika picha ya kwanza ya mtoto mpya aliyemzaa na nyota wa NFL, Stefon Diggs.
Huyo ni mtoto wa kwanza kwa wawili hao na Cardi B alichapisha picha zilizoleta hisia kali kupitia akaunti ya Instagram, ikionyesha kichanga hicho kikiwa mikononi mwake kwa upendo.
Kuanikwa kwa mtoto huyo wa Cardi B na Stefon Diggs imetajwa kama hatua muhimu katika safari ya familia ya wawili hao.
Mashabiki na watu mashuhuri walisherehekea tukio hilo, wakiwa na mchanganyiko wa furaha na shauku kuhusu jina la mtoto na maisha yake yajayo.
Cardi B, rapa mwenye Grammy ambaye nyimbo zake zisizo na woga zimepata nafasi ya juu kwenye chati za muziki duniani, huyo ni mtoto wa nne kwake na wa kwanza kwa mchumba wake Stefon Diggs, ambaye thamani yake ya mali ilionekana kufikia kiwango kikubwa baada ya mkataba wake na Patriots, huku Cardi B akiendelea na malezi ya pamoja na mumewe wa zamani, Offset.
Picha ya kichanga hicho na Cardi B iliyoshuhudiwa na mamilioni ya watu ndani ya saa chache, huenda ilipigwa hospitalini.