Buti la Burna Boy lazua balaa

Thursday September 02 2021
burna pic
By Mwandishi Wetu

Eee bwana mtu wangu wa nguvu moja kati ya story inayoendelea kuleta gumzo katika mitandao ya kijamii ni ya buti alilovaa msanii kutokea Nigeria Burna Boy kwenye show yake siku ya Ijumaa huko Uingereza katika ukumbi wa O2 Arena.Unaambiwa buti hilo limeendelea kuwa gumzo huko mitandaoni kutokana na muonekano wake wa kipekee.Msanii huyo anayetambulika kama African Giant alivalia buti hilo lililokuwa lina rangi nyeusi kutoka kampuni ya mavazi ya Rick Owens ya Marekani ambayo inajihusisha na ubunifu, uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mavazi yao ambayo yamekuwa maarufu kutokana na upekee wake.Mavazi hayo kwa kiasi kikubwa hutumiwa na watu maarufu kama models, wanamuziki na waigizaji kutokana na gharama kuwa juu na ndio maana ni nadra sana kuona watu wa hali ya chini wakitumia bidhaa zao.

Advertisement