Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basata yasitisha matamasha na burudani kwa siku 14

Basata yasitisha matamasha na burudani kwa siku 14

Muktasari:

  • Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kusitisha matamasha na burudani kwa siku 14 kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kusitisha matamasha na burudani kwa siku 14 kutokana na msiba wa aliyekuw Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Taarifa iliyotolewa na kaimu katibu mtendaji wa Basata, Matiko Mniko inasema baraza limewaelekeza wadau wake kusitisha vibali vya matamasha na burudani kwa siku 14 ili wananchi waungane kuomboleza msiba wa Magufuli.

Rais wa Tanzania John Magufuli afariki dunia

“Baraza limewaelekeza wadau wake kusitisha vibali vya matamasha na burudani kwa siku 14 kuanzia Machi 17 ili wananchi waungane kuomboleza katika kipindi hiki kigumu kwa Taifa,” imesema taarifa hiyo.

Rais Magufuli alifariki dunia juzi Jumatano Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akitangaza msiba huo, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema Rais Magufuli alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo.