Alichoahidi Rais Samia kwenye sanaa

Rais Samia Suluhu Hassan amesema  kwenye miaka hii mitano serikali inakusudia kuikuza zaidi sekta ya sanaa  hususani kwa kuimarisha usimamizi wa hati miliki ili wasanii waweze kunufaika na kazi zao.
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi ya Aprili 22, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Tanzania ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tangu kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania Machi 19 mwaka huu.
Katika hotuba yake hiyo pamoja na mambo mengine, amesema sekta ya Sanaa inakuwa kwa kasi kubwa ambapo vijana  wengi wamepata ajira kupitia sekta hiyo.
Rais Samia amesema  kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), watauuhisha mfuko wa sanaa na utamaduni ili  kuwasaidia wasanii ikiwemo kupata mafunzo na mikopo .
“Kwa hiyo tutajitahidi kuiangalia sekta hiyo angalau basi ipatwe msukumo na kupandisha ari," amesema Rais Samia