Wema kipotabo kama anakuja, anakataa vile

Friday September 11 2020
wema sepetu pic

Aisee! shida ya kuwa supastaa hasa wakati huu wa Instagram na Snapchat ni kwamba, maisha yako yanakuwa sio mali yako tena, bali ya wananchi wote.
Moja ya uthibitisho wa hii kitu inaweza kuwa ni kasheshe analokumbana nalo miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kupitia comment anazozipata katika kurasa yake ya Instagram kuhusu mwili wake.
Kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba, baada ya kuingia kwenye Bongo Movie, Wema aliongezeka mwili mpaka kufikia kilo 109, na akadumu na muonekano huo kwa muda mrefu kabla ya mwaka 2019 alipoamua kuchukua hatua ya kujipunguza zaidi.
Kwa sasa amerudi kwenye ule mwili wake wa Wema kipotabo, lakini kila anapoposti picha zake Instagram mahakama inachafuka kwa komenti zenye kupongeza na zingine zikiponda muonekano wake.
Moja ya komenti iliyotrend iliwekwa majuzi na shabiki mmoja ambapo ilimkera Madam Wema kiasi kwamba, alimsemea mbovu shabiki yake huyo kwa matusi ya nguo.
Kama hiyo haitoshi, katikati ya wiki hii, Steve Nyerere alipost picha inayowaonesha warembo watatu, muigizaji Kajala, Dayna Nyange na Wema wakiwa kwenye kampeni za CCM, lakini kilichotokea ni asilimia kubwa ya komenti hizo zilikuwa zinaunanga muonekano wa Wema huku chache zikimtetea — kwa hiyo imekuwa ni kama muonekano wake wa sasa unakuja, unakataa flani vile kwa watu wake.

Advertisement