Mwijaku afikishwa mahakamani akituhumiwa kusambaza picha za utupu

Wednesday July 29 2020

 

By Hadija Jumanne

Dar Es Salaam. Mtangazaji wa kampuni ya Clouds Media, Mwemba Burton maarufu Mwijaku (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusambaza picha za utupu.
Mwinjaku ambaye alikuwa mmoja wa watia nia jimbo la Kawe, amefikishwa mahakamani hapo leo, Julai 29, 2020 na kusomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.
Akisomewa shtaka lake, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Mwanaamina Kombakono, alidai kuwa mshtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 110.
Wakili Kombakono alidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar Es salaam.
Alidia katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapishwa picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliunganishwa katika Kompyuta.
Mshtakiwa amekana shtaka na amekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka ama Bongo Movie au tasnia ya muziki wenye barua zilizothibitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), ambao watasiani bondi ya Sh  500,000 kila mmoja.
Hakimu Kabate ameahirisha Kesi hiyo hadi Agosti 12, 2020 itakapotajwa.

Advertisement