Mdogo wa Kanumba amaliza mwendo

Saturday December 7 2019

Mdogo wa Kanumba amaliza mwendo-afariki-seth-uti wa mgongo-mlemavu-kifo-burudani-filamu-

 

By Rhobi Chacha

MDOGO wa aliyekuwa nyota wa filamu nchini, Steven Kanuimba Seth Bosco amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi, ikiwa ni miaka saba na miezi tisa tangu Kanumba alipofariki na kuzikwa jijini Dar es salaama baada ya kufa ghafla nyumbani.
Seth amekumbwa na mauti akiwa nyumbani kwa mama yake Kanumba, Mbezi Temboni jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa na maradhi aliyokuwa nayo.
Akizungumza na MCL Mama Kanumba amesema Seth alikuwa anaumwa kwa muda mrefu ugonjwa ambao ulianza kama masihara na matokeo yake ukawa mkubwa na kuwa Mlemavu wa miguu hadi   kufanyiwa upasuaji kwenye uti wa mgongo .
Mama Kanumba amesema Seth ameanza kuumwa akiwa Kanisani  kuna siku aliamka mzima  akamuaga anakwenda kanisani ,  Akiwa kanisani akainama kufunga kamba ya viatu, wakati ameinama akasikia kama shoti ya umeme mgongoni alivyorudi akamwambia alijisikia vibaya kanisani tokea hapo ndipo akawa mgonjwa hadi mauti kumkuta.
"Nimehangaika nae sana Seth ila Mungu amempenda zaidi, ameanza kuumwa kama utani matokeo yake ikifikia hadi hatua ya kuwa mlemavu wa miguu ,tulimpeleka Hospitali mbalimbali lakini ndio hivyo amefariki "alisema Mama Kanumba
Amesema Mama Kanumba mwili wa Seth kwa sasa umehifadhiwa katika Hispitali ya Taifa Muhimbili  taratibu zote za mazishi zinafanyika nyumbani Mbezi  Temboni.

Advertisement