Lulu Diva kuhamia mazima kwenye filamu

Tuesday May 5 2020

 

By RHOBI CHACHA

MSANII wa muziki Bongo Flava nchini, Lulu Diva ambaye anafahamika zaidi kwenye  nyimbo kama Utamu, Ona, Amezoea, Nilegeze na nyingine amesema anajuta kuchelewa kuingia kwenye sanaa ya maigizo kwani huko ndio kipaji chake halisi kilipo.
Lulu Diva amezungumza na Mwanaspoti Online amesema, itafikia muda ataacha kuuimba ili ajikite zaidi kwenye kuigiza ili aweze kuonesha uhalisia wa kipaji chake alichonacho na sio muziki.
“ Ukweli kwa muda mfupi niliofanya  Tamthilia ya Rebecca nimegundua kujuta kuchelewa kuingia kwenye sanaa ya maigizo, huku ndio kwenye kipaji changu na nimepata mashabiki wengi kuliko kwenye muziki, hivyo itafikia muda nitahamishia nguvu zangu zote kwenye kuigiza na naamini nitafika mbali" amesema Lulu Diva.

Advertisement