Kadinal Jento aachia sebene

Friday December 6 2019

 

By Rhobi Chacha

Mwalimu na mkongwe wa kuibua vipaji katika Nyumba ya Vipaji Tanzania(THT) Kadinal Jento ameachia Sebene zikiwa zimebaki siku 25 kumalizika kwa mwaka 2019.
Sebene hilo ambalo wameshirikishwa Marapa wakongwe Totoo Ze Bingwa na Sauti ya Radi huku Kadinal Jento mwenyewe  amesimamia shoo nzima ya midundo ya muziki katika Sebene hilo.
Akizungumza na MCL Digital Kadinal Jento ambaye amechangia kukuza vipaji vya wanamuziki Ben Pol, Barnaba, Amini, Linah, Rachel, Maunda Zorro, Mwasiti, Ruby, Nandy, Barnaba, Ditto na wengine wengi amesema, kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kutoa nyimbo, ameamua  kutoa zawadi aliyowaandalia mashabiki zake katika kufunga mwaka.
Kadinal Jento alianza kutamba na kibao chake Mundende, Dhahabu,Kula kuku mayai ,alianza kuwa mwalimu THT toka mwaka 2005 hadi sasa, na kabla hajajiunga na chuo hicho alipofika Tanzania mwaka 1994 alijiunga na FM Academia na baadae akishirikiana na mwanamuziki Ndanda Kosovo wakaanzisha bendi ya Stono Musica 'Wajelajela'

Advertisement