Daz Baba afunguka ukimya wake

Tuesday May 5 2020

 

By RHOBI CHACHA

BAADA ya kimya cha muda mrefu, Msanii wa Bongo Bleva aliyetamba miaka hiyo na ngoma kama 'Nipe tano' , 'Namba nane' na nyingine nyingi Daz Baba ameeleza sababu ya ukimya wake.
Akizungumza na Mwanaspoti Online leo Jumanne, Daz Baba, amesema ukimya wake ni kwa sababu ya kujipanga zaidi kimuziki pia ni kukwepa vita na binadamu na kutafakari mambo yaliyopita kwenye maisha yake.
“Unajua nipo kimya kwa sababu napanga mambo yangu mengi na kingine sihitaji vita na binadamu ukiwa kimya hiyo inasaidia usikumbane na mambo ya ajabu, sasa hivi namtumainia aliye juu tu na si kingine,” amesema Daz Baba
Daz Baba aliwahi kuwa mmoja wa kundi la  muziki Daz Nundaz Family  ambalo lilipata umaarufu miaka ya 2000 lilikuwa likiundwa na Feruz, Sajo, La Rhumba, Daz Baba na Critic.
Wimbo wake wa mwisho kuutoa kwa video ni Karibu Tanzania aliouachia mwaka ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuvutia utalii nchini.

Advertisement