Aliyepora simu ya Mama Diamond akiona cha moto

Saturday November 9 2019

Aliyepora -simu- Mama -Diamond -akiona - moto-Viwanja - Posta-ameibiwa - Simu -wasafi-festival-Mwanaspotiburudani-

 

By Rhobi Chacha

MAMA mzazi wa staa wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Bi Sandra maarufu kama Mama Diamond ameibiwa  Simu  katika Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam, lakini aliyehusika na tukio hilo amekiona cha moto baada ya kushushiwa kipondo hevi.
Tukio hilo limetokea jioni ya janawakati wasanii wakiwa wanafanya  Sound Check Kwenye Jukwaa La Wasafi festival kwa ajili ya Tamasha litakalo fanyika kesho Septemba 9, 2019.
Mama Diamond alifika katika viwanja hivyo akiwa ameongozana na mumewe Shamte na aliyekuwa Mkurugenzi wa African Stars 'Twanga Pepeta ' Asha Baraka, akiwa anashuka kwenye gari watu walimzunguka ndipo akatokea kijana mmoja alipomvamia na kumpora simu kisha kukimbia.
Kijana huyo  hakupiga hatua hata kumi kabla ya kuvamiwa na kundi la watu na kuanza kumpiga baada ya kumnyang'anga simu na kama sio askari polisi waliomuokoa habari ingekuwa nyingine.
Baada ya hapo Mwanaspoti liliongea na Mama Diamond kuhusu tukio hilo, ambapo amesema, amejikuta amezungukwa na kundi la watu baada ya kufika katika eneo hilo na kuporwa simu na kijana  huyo asiyemfahamu.
"Mimi hadi sasa sielewi, maana nimefika tu hapa, naona watu wamenizunguka kwenye gari yangu, nafungua mlango wamesogea ndipo yule kijana akanisogelea karibu yangu na kunipora  simu," alisema Mama Diamond.
Hata hivyo Mama Diamond aliwaomba polisi wamsamehe  kijana hiyo kwakuwa simu yake imerudi ila Polisi waligoma.

Advertisement