Alicia Keys aingia studio kuimba singeli

Saturday February 22 2020

 

By Nasra Abdalah

ILE ndoto ya kuhakikisha muziki wa singeli unapaa kimataifa inaelekea kutimia baada ya msanii wa Marekani, Alicia Keys kuingia rasmi katika miondoko hiyo.
Alicia anafanya hivyo ikiwa ni siku chache tangu mume wake, Swizz Beatz kuweka vipande vya wimbo wa singeli wa ‘Wanga’ uliombwa na msanii Meja Kunta akimshirikisha Lavalava kutoka lebo ya WCB.
Swizz Beatz ambaye ni mume wa Alicia, ameonyesha kuvutiwa na aina hiyo ya muziki na kumuingiza mkewe studio kufanya (remix).
 Akiwa studio Alicia aliyevaa koti la rangi ya kaki, fulana ya pullover ameonekana akicheza wimbo huo kwa madaha kama Mswahili wa katikati ya viunga vya jiji la Dar.
Chini ya video hiyo aliyoitupia katika ukurasa wake wa instagram, aliandika ‘Big Zone’.
Alipouliza meneja wa  WCB, Hamis Tale maarufu Babu Tale amesema kuwa “Ni makubaliano kati yetu wameupenda wimbo huo na wakaomba kuufanyia remix, tukatae sisi nani” amesema Tale huku akihoji.

Advertisement