Yondani, Abdul warejea Yanga, Dante bado

Tuesday August 13 2019

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Mabeki Kelvin Yondani na Juma Abdul ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliondoka alfajiri ya leo (Jumanne) kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki ili kuzoea mazingira ya baridi.

Habari njema kwa Yanga ni kurejea kundini kwa mabeki wake Yondani na  Abdul baada ya kukaa nje kwa muda wakishindikza kulipwa malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili.

Mwanaspoti linafahamu Yondani amepewa fedha Sh 11 milioni alizokuwa anadai, huku Juma Abdul akiambiwa arejee kambini kisha uongozi utazungumza naye kuweza kumlipa pesa zake.

Kwa upande wa Andrew Vicent 'Dante', inatajwa mchezaji huyu bado hajatafutwa na kiongozi yoyote yule kuhusu kulipwa malimbikizo yake ya pesa usajili (Pesa nzima ya usajili), baadayr mchezaji huyo tangu msimu uliopita kutochukua.

Huku beki Paul Godfrey 'Boxer' yeye ameachwa katika msafara huo kutokana na maumivu aliyoyapata katika mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Township Rollers.

Yanga inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Polisi Tanzania Agosti 16, mkoani Arusha.

Advertisement

 

 

 

Advertisement