Yanga wateua wajumbe wapya

Muktasari:

YANGA ndio klabu iliyotwaa mara nyingi taji la Ligi ya Bara ikifanya hivyo mara 27 tangu mwaka 1965 ikifuatiwa na Simba yenye mataji 20 kwa sasa.

SIKU chache tangu wajumbe watatu wa kamati ya utendaji ya Yanga kujiuzulu na wengine wawili kusimamishwa, mabosi wa klabu hiyo wameteua wajumbe wapya wawili wa kuziba nafasi hizo, huku ikimtangaza Hamad Islam kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Yanga inasema Kamati ya Utendaji chini ya Mwenyekiti wake Dk. Mshindo Msolla imewateua Suma Mwaitenda na Haruna Batenga kuziba nafasi mbili kati ya tatu zilizoachwa wazi na waliojizulu akiwamo Shija Richard, Said Kambi na Rodgers Gumbo.
Aidha kamati hiyo imewateua, Hamad Islam kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano iliyokuwa chini ya Gumbo na pia kumtangaza Dominic Albinus kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi akichukua nafasi ya Salim Rupia aliyesimamishwa na kamati ya Utendaji.
Dominic awali alikuwa makamu mwenyekiti hiyo ya ufundi.