Vimba ya Isha Mashauzi kutoka wiki hii

Tuesday July 16 2019

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Mmiliki na mwanamuziki wa kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani maarufu ‘Isha Mashauzi’ amesema anatarajia kutoa wimbo wake mpya utakaoitwa Vimba wiki hii.

Isha amesema hayo baada ya mashabiki zake kumshauri atengeneze wimbo mwingine unaomuhusu mama kutokana na kufiwa na mama mwezi mmoja uliopita.

Aidha Isha aliyewahi kuimba wimbo unaojulikana kwa jina la mama ambao aliimba na marehemu mama yake bi Rukia Juma, amewaambia mashabiki zake kuwa, kwa sasa anahitaji muda wa kupumzika wa kutoa nyimbo hivyo hawezi kutengeneza wimbo mpya kwani hata vimba utakotoka wiki hii ameutengeneza miezi sita iliyopita.

"Nashukuru mashabiki zangu kwa kunipa ushauri wenu wa kutaka nitunge wimbo mwingine unaohusu mama, ila naomba niwaambie kuwa sitaacha kumuimbia mama ila tu nahitaji muda kwani sina utulivu kwa sasa, naweza kutengeneza wimbo mpya nikauharibu hivyo mniwie radhi maombi yenu nitayafanyia kazi nitakapo kuwa sawa

"Najua mtajiuliza kwanini nimetangaza wiki hii nitatoa wimbo mpya unoitwa Vimba, huu wimbo ni liutengeneza miezi sita iliyopita na kwa bahati mbaya hata matukio ya video nimeshindwa kuyakamilisha hivyo nitaanza na Audio kwanza halafu video itaguata baadae."

Advertisement