Timu sita zaviziana nafasi moja kupanda, Pamba yanukia Ligi Kuu

Wednesday May 15 2019

 

By Charity James

NI timu mbili hadi sasa zimetangazwa kupanda daraja ambazo ni Namungo FC na Polisi Tanzania leo kuna mchezo mmoja kati ya Mbeya Kwanza dhidi ya Pamba ambao ni maalumu kwa ajili ya mchujo kupata timu moja inayotakiwa kupanda.

Ni timu sita zinazowania nafasi hiyo moja ambapo baada ya mchezo huo wa leo Geita dhidi ya Mlale kisha kurudiana Mei 22.

Mshindi wa kati ya Mbeya Kwanza na Pamba atapambana na timu itakayokamata nafasi ya 18 TPL huku mshindi baina ya Geita na Mlale atavaana na timu ya 17 TPL, na mshindi wa kila upande watapambana kupata mshindi mmoja wa kwenda Ligi Kuu ili kukamilisha idadi ya timu tatu.

Katika mchujo huu endapo timu ya TPL inashindwa basi itashuka FDL lakini zile za FDL zikishindwa zitabaki.

Pia wakati Mgambo na Kiluvya zikiwa zimeshuka kwenda Ligi Daraja la Pili (SDL), timu zilizomaliza nafasi ya 10 na 11 kwa kila kundi nazo zitacheza 'play off' ili kupata timu moja itakayoshuka daraja wakati kule TPL yule wa 19 na 20 watakuwa wameshuka moja kwa moja.

Advertisement