Tecno yaongeza mkataba na Man City

Friday July 19 2019

 

By Daniel Francis

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tecno ya nchini China imeongeza mkataba wake na klabu ya Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).
Katika mkataba huo uliosainiwa India, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Stehen Ha amesema, “Tecno ina furaha kuwa brandi yetu na itavaliwa na Manchester City katika mashindano ya Asian Trophy na tunaamini kuwa na ushindi pamoja na rangi ya bluu vitasaidia kushinda”.
Pia kupitia ushirikiano huo Makamu Raisi wa ushirikiano Manchester City, Damian Willoughby alisema, “Manchester City inayofuraha kutangaza rasmi mkataba uliosainiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kampuni ya TECNO umesainiwa tena, Kampuni inayoongoza Afrika na Asia TECNO, tumeshirikiana nao kwenye mambo mengi ya kimpira na biashara, ni jambo zuri kuwa bado tunaendelea nao hasa katika mashindano ya Asian Trophy “ alisema Damian.
Mkataba huo umeanza kuonesha mafanikio mapema ambapo mabingwa hao wa ligi ya Uingereza, Manchester City waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya West Ham na kutinga fainali katika mashindano ya Asian Trophy yanayoendelea China ikiwa pia ni maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao.

Advertisement