Ratiba Simba wala siyo tatizo

Wednesday April 24 2019

 

By Thobias Sebastian

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema ugumu wa ratiba waliyokuwa nayo wala hauna shida kwake na kuna mbinu ambazo atazifanya ili kuhakikisha kila mchezo uliokuwa mbele yao wanapata ushindi.

Kocha huyo alisema malengo yake ni kushida na kuvuna pointi tatu ili kufikia malengo yao ya kutetea ubingwa msimu huu.

Alisema ili kukabiliana na ratiba ya kucheza mechi kila baada ya siku mbili mpaka tatu nitakuwa nafanya mabadaliko ya kikosi kulingana na wachezaji ambao nitakuwa nimewatumia kwenye mchezo uliopita nitawapumzisha na unaofata nitatumia wengine.

"Hatuna muda wa kutosha kufanya mazoezi ila nitautumia ila mchache uliokuwepo nitatumia katika kuewaelekeza zaidi wachezaji wangu na wale waliotumia sana nao kupata muda wa kupumzika ili siku ambayo nitawatumia kupata nafasi ya kucheza vizuri," alisema Aussems.

Nahodha wa Simba John Bocco alisema kimsingi kwao wana ratiba ngumu ambayo inawakabili kipindi hiki kucheza mechi kila baada ya siku mbili mpaka tatu wachezaji wanatakiwa kushindani zaidi pengine hapo awali.

Bocco alisema benchi la ufundi limeliona hilo na litakuwa linawapa mbinu na hata mabadiliko ambayo yanafanyika katika kila mechi anaungana nayo ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kupumzika kwani hata wale ambao wanapata nafasi ya kucheza hawata fanya mzaha hata kidogo.

Advertisement

 

 

 

Advertisement