Rashford, Maguire wabishana uwanjani

Manchester, England. Nahodha wa Manchester United, Harry Maguire amegombana na mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford kutokana na kadi ya njano aliyoonyeshwa Erik Lamela.

Lamela alionekana kama alianza kumpiga Anthony Martial, jambo ambalo liliamhs ahasira za mchezaji huyo wa Ufaransa ambaye alirudishia na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Man United na Spurs, alimwonyesha kadi nyekundu Martial, lakini alimwonyesha Lamela ya njano, katika mchezo ambao Spurs ilikitandika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer mabao 6-1.

Katika tuki hilo, ambalo lilinaswa na kamera pamoja na sauti zao zikisikika kwa nahodha wa ManUnited, Maguire akibishana na Rashford juu ya kama Lamela naye kuonyeshwa kadi nyekundu au la.

Rashford alisikika akimlaumu nahodha wake kwa kushindwa kulisimamia hilo akisema: “Hakuna lolote juu ya kiwiko alichopiga (Lamela)?

Aliuliza mshambuliaji huyo baada ya mwamuzi Anthony Taylor kumfuata Lamela na kutoa kadi ya njano.

Rashford aliendelea: “Kwanini na tukio na matukio yanafanana?” Maguire akamjibu: “Siyo kama lile, wameangalia katika VAR.”

Lakini Rshford alisisitiza: “Amempiga kiwiko!’ Na nahodha wake alimaliza kwa kumwambia: “Wameangalia na hakuna hilo unalosema.”