Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba bado aiweka roho juu Manchester United

Muktasari:

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka England

London, England. Paul Pogba ameiweka njiapanda Manchester United kuhusu usajili wake wa majira ya kiangazi.

Licha ya kucheza kwa kiwango bora katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England walioshinda mabao 4-0 dhidi ya Chelsea, Pogba hajatulia.

Pogba alisema muda ukifika utaamua atakuwa klabu gani, kauli ambayo inaonyesha bado ana dhamira ya kuondoka Old Trafford.

Real Madrid imekuwa ikimuwinda mchezaji huyo wa Ufaransa katika usajili wa majira ya kiangazi.