Tausi atoboa siri ya kuficha ujauzito wake

Friday January 10 2020

Mwanaspoti-Tausi-Tanzania-bongo-atoboa siri-kuficha-ujauzito-wake

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam.Mwingizaji Tausi Mdegela ametoa siri ya kuficha ujauzito wake akihofia asije akaiibiwa na wanawake wenye tabia za 'nyakunyaku'.

Tausi amejifungua mtoto wa kike Januari 8 mwaka huu katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Hospitali ya Amana, Tausi kuhusu suala la hilo alisema aliamua kuficha ujauzito wake kutokana na umbile lake ili kuepusha maneno ya watu, pia mwanaume wangu ni 'Handsome' nahofia wasije niibia wanawake wenye tabia za 'nyakunyaku'.

"Nashukuru nimejifungua salama mtoto wa kike, nimejifungua kwa njia ya upasuaji hivyo kesho natarajia kutoka Hospitali, niliamua kuficha ujauzito wangu kutokana na umbile langu niliona nisiutangaze ili kuepusha maneno ya watu, ona kama hivi tu nimetuma picha nilipokuwa na ujauzito maneno kibao kila mtu anasema lake" alisema Tausi

Aidha Tausi hakuta kuweka wazi baba wa mtoto huyo ambapo amesema hapendi maisha yake binafsi na hata muhusika hapendi mambo ya mitandaoni.

"Kiukweli siko tayari kumuweka wazi mwanaume niliyezaa naye, sababu sio mtu wa mitandao na hatupendi watu watujue maisha yetu binafsi, halafu kingine mwanaume wangu ni 'Handsome' bwana nahofia wasije niibia wanawake wenye tabia za 'nyakunyaku'," alisema Tausi

Advertisement

Aidha Tausi anawashukuru watu wote waliokuwa pamoja naye kipindi chote cha ujamzito na hadi sasa amejifungua.

Advertisement