Morrison apewa ndinga

Tuesday September 15 2020

 

By MWANDISHI WETU

WINGA wa Simba, Bernard Morrison raia wa Ghana ameushukuru uongozi wa Simba kwa kumpa gari ya kutembelea aina ya Nissan Fuga yenye thamani ya kati ya Sh 14 na 15 milioni.

Morrison ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuliweka gari hilo huku akiandika maneno kwa lugha ya kiingereza ambayo yalikuwa na maana hii; "Ahsante bosi Mo Dewji, wewe ni kiongozi mkubwa, ahsante Simba, mnajua kutunza vizuri wachezaji wenu,"

Kati ya nyota hao, Morrison ambaye amesajiliwa akitokea Yanga ameonekana kuwa mwenye furaha kubwa ambayo ameionyesha wazi katika kushukuru.

Morrison ametua Simba ambapo usajili wake ulikuwa na utata hadi kupeleka Kamati ya Sheria, Hadhi na Haki za wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini kuingilia kati na kutoa uamuzi wa kwamba mchezaji huyo yupo huru kwani mkataba wake na Yanga ulikuwa na mapungufu.

 

Advertisement