Mauya amwaga wino Jangwani

Friday July 31 2020

 

By Yohana Challe

MAMBO yameanza kunoga huko Mtaa wa Jangwani, baada ya uongozi wa Yanga kunasa saini ya Zawadi Peter Mauya.

Mauya amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akitoka Kagera Sugar ambayo imemaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.

Kagera imeendelea kubomoka, kwani saa chache zilizopita kiungo mwingine wa timu hiyo, Awesu Awesu alikuwa amesaini Azam FC.

Mauya kutoka Morogoro, alijiunga na Kagera Sugar akitokea Lipuli FC ya Iringa.

Mauya alikuwa ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Lipuli msimu uliopita wa ligi huku akifunga magoli matano.

Mauya anayemudu kucheza nafasi nyingi uwanjani, aliwahi kucheza Sabasaba United (Moro), Bukina FC (Moro), Rhino FC (Tabora FC) na Mufindi FC ( Iringa).

Advertisement

 

Advertisement