Maguire kuvunja rekodi ya mabeki wiki hii

Wednesday June 26 2019

 

BEKI wa Leicester City na Timu ya Taifa ya England, Harry Maguire, 26, anajiandaa kuwa beki ghali zaidi duniani kwa kujiunga na Manchester City ambayo itavunja benki na kutoa dau la Pauni 80 milioni kwa staa huyo na kuipiku Manchester United inayomtaka kwa udi na uvumba.

Kwa dau hilo Maguire atavunja rekodi ya uhamisho iliyowekwa na beki wa Liverpool, Virgil van Dijk ambaye alinunuliwa kwa dau la Pauni 75 milioni akitokea Southampton katika dirisha la Januari mwaka jana.

Kocha wa City, Pep Guardiola ameamua kumnunua Maguire kwa ajili ya kuziba pengo la beki wake, Vincent Kompany ambaye amerudi nyumbani kwao Ubelgiji na Manchester City itamlipa Maguire dau la Pauni 280,000 kwa wiki.

Hivi karibuni beki huyo wa Leicester City alikaririwa akiwaambia marafiki zake kuwa atatua Man City,Man United ilikiuwa ikimtaka beki huyo tangu enzi za Kocha Jose Mourinho.

Advertisement