Kisu: Corona inatufunza maisha

Friday April 10 2020

 

KIPA wa Gor Mahia ya Kenya, Mtanzamia David Kisu amesema kipindi alichokaa nyumbani kimemfunza kusaka plani B nje na soka.

Ligi ilisimama duniani kote ili kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona, jambo hilo limekuwa funzo kwa Kisu kusoma alama za nyakati.

"Hiki kipindi kimekuwa kigumu kupita maelekezo kwasababu unatumia pesa, huingizi pesa hapa lazima mtu ujichanganye kujua namna ya kusaka plani B,"

"Kila jambo linapokuja lazima kujifunza kitu ndani yake, mfano mtu ambaye alikuwa anategemea kazi moja anakuwa na wakati gani kwa sasa na ndio maana nimesema lazima tujifunze kuwa na plani B,"amesema.

Amesema kupitia kazi yao ya soka nje na mshahara kuna posho za hapa na pale  wanazozipata zinazokuwa zinawasaidia kimaisha.

"Kukaa nyumbani muda mrefu inatufanya tuwe tunajibana matumizi yetu hapa tutajifunza kuwa na plani B,"amesema.

Advertisement