Kishindo kikubwa usajili Yanga

YANGA iko kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga wa zamani wa CD Teneriffe ya Hispania, Farid Mussa ambaye ataingia kambini na wenzake Jijini Dar es Salaam Jumatatu ijayo lakini Kamati ya Ufundi imetangaza kishindo kingine.

Mbali na Farid tayari Yanga imeshamsainisha Abdallah Shaibu ‘Ninja’ mkataba wa miaka miwili huku ikimalizana na mido wa Azam, Aboubakary Salum ‘Sure Boy’ ambaye klabu yake imeshamruhusu kumalizana na Yanga.

Juzi Yanga iliandika barua kumuomba mchezaji huyo ambaye kwa karibu misimu mitano sasa kila dirisha la usajili linapofunguka amekuwa akihusishwa na Jangwani ambako ali-cheza baba yake zamani.

Taarifa rasmi ya Yanga jana ilisema wachezaji wote wapya na wale wa zamani wataingia kambini Jumatatu kujinoa na msimu mpya kwani muda ni mfupi. Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinus ametangaza rasmi kwamba kuna kishindo kikubwa kinakuja kwenye usajili wa kikosi hicho ambao hautazidi wachezaji 25.

Amesisitiza kwamba mashabiki watarajie usajili wa majina makubwa kushinda yale ambayo wameshayasikia mpaka sasa huku akidai kwamba “Ni rasharasha tu, bado mvua haijanyesha.”“Tunaleta mchezaji ambaye kwa sifa na takwimu zake za uwanjani, kila mtu aseme kweli huyu ni mchezaji,” alisema.

“Tukisema mchezaji ni mchezaji kweli, kwak-weli itakuwa ni mtikisiko mkubwa, tunataka kurudi kwenye ule utamaduni wetu kwamba ukienda uwanjani ni suala la kuhe-sabu magoli tu, kwamba uulize tumeshinda mabao mangapi, si kuwa na wasiwasi na ushindi,” alisisitiza Albinus.

Yanga imemrejesha rasmi Ninja akitokea MFK Vyskv ya Czech lakini ikafichuka kwamba jamaa ndio anapewa nafasi ya mkongwe Kelvin Yondani.

Ninja amesaini mkataba wa miaka miwili jana mchana ukiwa ni usajili wa tatu wa Yanga kwa upande wa mabeki akitanguliwa na Bakari Mwamnyeto (kutoka Coastal Union) na Yassin Mustapha (kutoka Polisi Tanzania).

Beki huyo ambaye amewahi kuitumikia kwa mkopo LA Galaxy ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), anarejea Yanga baada ya kuachana nayo kwa miaka miwili kutokana na mkataba wake kumalizika.

Yanga imelazimika kumsajili Ninja baada ya kukosa saini ya beki mwingine wa Coastal Union Ibrahim Ame ambaye juzi alisain-ishwa kimafia na Simba ikimchukua juu kwa juu wakati akiwasili bandarini akitokea Zanzibar.Usajili wa Ame ulikuwa ni maalum kuja kuchukua nafasi ya Yondani ambaye mazungumzo yake ya kuongeza mkataba bado yanasuasua.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ndogo ya usajili ni kwamba kusaini kwa Ninja kuna-zidi kuweka shaka ya uwezekano wa Yondani kupewa mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Wengine waliosaini Yanga mpaka sasa ni kiungo Zawadi Mauya (Kagera Sugar) na mshambuliaji Waziri Junior (Mbao).

WAMEACHWA

Mrisho Ngassa, David Molinga, Jaffary Moham-med, Tariq Seif, Andrew Vicent ‘Dante’, Patrick Sibomana, Papy Tsh-ishimbi na Mohammed Banka.

MAZUNGUMZO KUSITISHA MIKATABA

Ally Sonso, Muharami Maundu, Ali Ali, Yikpe Gislain, Eric Kabamba na Rafael Daudi.

 UHAKIKA KUBAKI

Farouk Shikhalo, Ram-adhani Kabwili, Metacha Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Bernard Morri-son, Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyum Saleh, Said Makapu, Mapinduzi Balama, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Ab-dulaziz Makame na Paul Godfrey. Mazungumzo ya kuongeza mikataba ya Yondani na Juma Abdul yanaendelea. Albinus alipoulizwa kuhusu dili la kocha Ndayiragije Ettiene, alisema mchakato unaendelea.