Imeisha hiyo, tukutane nusu fainali Europa

Wednesday August 12 2020

 

DUISBURG, UJERUMANI. JANA hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League imefikia tamati baada ya kupigwa michezo miwili, ambapo Sevilla ikiwa katika dimba la  Schauinsland-Reisen-Arena  ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichabanga Wolves  bao 1-0.

Sevilla inakuwa imeweka rekodi yakuwa imecheza jumla ya mechi 18, katika michuano yote bila ya kupoteza, pia ikaweka rekodi ya kupata ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Wolves ambayo pia ilikutana nayo kwa mara ya kwanza.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Shakhtar Donetsk dhidi ya FC Basel ambapo Shakhtar Donetsk ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

baada ya michezo hiyo rasmi sasa Sevilla itakuwa inakwenda kukutana na Manchester United tarehe 16, mwezi huu katika hatua ya nusu fainali , huku Inter itakuwa inaumana na Shakhtar Donetsk tarehe 17 mwezi huu.

Michezo yote inatarajiwa kupigwa saa 4:00 usiku na hakutakuwa na michezo ya marudiano mshindi katika mechi hizo atakuwa anaingia moja kwa moja katika hatua ya fainali.

Hatua hiyo ya fainali inatarajiwa kupigwa 12, mwezi huu, katika Uwanja wa Stadion Koln katika Jiji la Cologne huko nchini Ujerumani.

Advertisement

Advertisement