Cioaba atuma salamu Mbao FC

Saturday November 16 2019

 

By Thomas Ng'itu

KOCHA wa Azam FC, Aristica Cioaba amewatumia salamu Mbao FC baada ya kikosi chake kuifunga Friends Rangers mabao 6-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Jumamosi asubuhi uwanja wa Chamazi.
Katika mchezo huo Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walishindwa kuonyesha cheche mbele ya wapinzani wao kinachonolewa na Mromania huyo.
Mabao ya Azam yalifungwa na Mudathir Yahya, Idd Kipagwile, Donald Ngoma na Kassim Hamis aliyefunga 'hat-trick'.
Mchezo huo ulikuwa maalumu kwa timu zote kujiweka fiti kipindi hiki cha mapumziko mafupi kupisha michezo ya timu za Taifa zinazocheza mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 kabla ya ligi zao kuendelea.
Azam waatanza mechi yao ya ligi baada ya mapumziko dhidi ya Mbao FC mchezo utakaochezwa Novemba 23 mwaka huu uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Advertisement