Bosi mpya Simba kuanza na haya

Muktasari:

Simba imemtambulisha Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa kuchukua majukumu yaliyoachwa na Crecsentius Magori ambaye ameaga rasmi.

BAADA ya Afrisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa kutamburishwa leo Jumamosi ametaja vipaumbele vyake vikubwa atakavyoanza navyo kubwa ni kuwafanya mashabiki na wanachama wateja kwa ajili ya maendeleo ya klabu.
Mazingisa ambaye ametambulishwa amechukuwa nafasi iliyoachwa na Clecsentus Magori ambaye anakwenda kufanya majukumu mengine.
Kipaumbele cha kwanza ni kuongoza kwa uhuru ndani ya sekretarieti yake, pia anataka kuongeza idadi ya vikombe kwenye klabu hiyo kwa timu zote kuanzia za vijana na wakubwa.
"Kuipeleka Simba kimataifa ijulikane dunia nzima na isiwe Afrika tu  kama inavyozungumzwa sasa lakini pia, kuiendeleza timu kibiashara ili klabu iweze kujiendesha yenyewe kama kulipa mishahara wachezaji na mambo mengine,"alisema Mazingisa.
Aliongeza, kuwafanya wanachama na wapenzi wa Simba kuwa wateja na si washabiki tu kwa ajili ya kuipa klabu maendeleo.
Alisema, kufanikiwa mambo hayo yanatakiwa umoja na ushirikiano kwa sababu kitendo cha mabadiliko siku zote huwa na changamoto.
"Lakini, tunatakiwa kutetea ubingwa wetu wa Ligi Kuu, kufanya vizuri kwenye FA, Kombe la Mapinduzi na mashindano mengine ambayo Simba itashiriki,"alisema Masingiza.
Aliweka namna namna alivyoshangaa siku ya sherehe za Simba Day baada ya kuona sehemu kubwa ya mashabiki wamejitokeza uwanjani kwa ajili ya kuishangilia timu yao.