Bosi mpya Simba humwambii kitu kwa Manara

Muktasari:

Senzo Mazingisa anakuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba wa pili tangu cheo hicho kitangazwe klabuni hapo baada ya Clecsentus Magori aliega leo Jumamosi.

AFISA Habari wa Simba, Haji Manara nyota yake ni kama inang'ara zaidi kwa bosi mpya wa Simba, Senzo Mazingisa baada ya kumkabidhi rungu la uhamasishaji.
Senzo ambaye kwa sasa ni Afisa Mtendaji wa Simba aliyechukua nafasi ya Clecsentus Magori aliyemaliza muda wake na sasa anakwenda kufanya majukumu mengine.
Alisema, anafurahi kumwona  Manara namna anavyokubalika na anavyofanya kazi ya uhamasishaji kwa mashabiki kuipenda timu yao na kujaa uwanjani.
"Nimekuwa nikimfuatilia kwa ukaribu Haji Manara ndivyo inavyotakiwa. Mambo anayofanya kwenye vyombo vya habari ni mazuri hivyo unatakiwa kuendelea hiyo. Wahamasishe mashabiki na wanachama wa Simba wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuishangilia timu yao,"alisema Senzo.
Alisema, mashabiki na wanachama hao wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kwa wachezaji ambao wanajiona wana majukumu ya kufanya vizuri kutokana na morali inayotoka kwao.
Hata hivyo, licha ya kauli ya kiongozi huyo kufafanua hiyo, hakuna taarifa mpya baada ya kusema huenda Manara kibarua kitaota mbawa na nafasi yake ikachukuliwa na mtu mwingine.