Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miquissone awatuliza mashabiki wa Simba SC

Muktasari:

Luis alisisitiza kwa kuwataka mashabiki wa Simba watulie na kwamba watakaporejea kwenye hali ya kawaida na kucheza wataipata burudani wanayoikosa kwa sasa, lakini akiwataka kila mmoja kujihadhari kwa kufuata maelekezo ya wataalamu kwa sababu virusi vya Corona vinaweza kuondoa maisha ya mtu kwa haraka pengine kuliko hata magonjwa mengine.

ACHANA na namna inavyowachanganya wananchi mpaka viongozi wa nchi kutokana na kasi yake ya duniani na jinsi inavyoathiri shughuli zikiwamo za kiuchumi, kijamii na hata kimichezo, nyota wa Simba, Luis Miquissone naye hajaachwa salama akiwa kwao Msumbiji.
Supastaa huyo aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo, amefichua kwa wiki chache ambazo amekaa nyumbani bila ya kucheza soka, ikiwa ni hatua ya kupunguza maambukizi ya virusi vya corona  tayari ameanza kuhisi kuumwa kutokana na kumisi kucheza mchezo huo.
Nyota huyo anayetajwa atawekwa karantini mara atakaporejea nchini akitokea Msumbiji kwa maangalizi ya afya yake, aliliambia Mwanaspoti kutoka Maputo kwamba, kusimama kwa ligi na kushindwa kuendelea kukinukisha kumechanganya licha ya ukweli ni jambo lisiloepukika.
Alisema kinachomfanya ajihisi kuumwa ni kwa vile ligi hiyo, imesimama wakati tayari alishaanza kulizoea soka la Tanzania na damu yake ilikuwa ikichemka alipokuwa akikukuruka uwanjani na wenzake, lakini kwa sasa hali kwake imekuwa ya unyonge kwa vile hachezi.
“Afya ya kila mmoja ni muhimu kuliko kitu kingine, lakini kiukweli nahisi kumisi kucheza soka, naamini tutapita salama katika kipindi hiki ili tuendelee na maisha yetu ya kawaida, licha ya kwamba najifua ndani kwa ndani, lakini nahisi kuna kitu nakosa,” alisema nyota huyo ambaye amepachikwa jina la utani, Konde Boy.
Luis alisisitiza kwa kuwataka mashabiki wa Simba watulie na kwamba watakaporejea kwenye hali ya kawaida na kucheza wataipata burudani wanayoikosa kwa sasa, lakini akiwataka kila mmoja kujihadhari kwa kufuata maelekezo ya wataalamu kwa sababu virusi vya Corona vinaweza kuondoa maisha ya mtu kwa haraka pengine kuliko hata magonjwa mengine.
“Pamoja na kumisi kwangu mpira naunga mkono kampeni ya kila mtu kukaa nyumbani kipindi hiki ili tuondokane na corona,” alisema.
Wakati huo huo, Kuna picha ambayo ilionekana kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha bwana mdogo mmoja akiwa amevalia T-sheti ambayo imechorwa mgongoni jina la mchezaji huyo wa kimataifa wa Msumbiji imempa faraja kubwa winga huyo matata.
Luis aliizungumzia jambo hilo, alisema, “Kila kitu kipo sawa kwa sababu tumepata mawasiliano naye hivyo atafikishiwa jezi orijino kama nilivyoahidi na kazi hii itafanywa na taasisi yangu huku nami nikienda kama itawezekana Morogoro kumuona, amenisisimua sana,” alisema Luis.
Inaelezwa mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 6-9 ni mkazi wa Morogoro na Luis alisema alishapata mawasiliano wa kufanikisha jambo hilo.

AMTAJA UHURU
Usione Konde Boy ndani ya muda mfupi amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba, Luis amefichua kuwa maujanja yote na siri za soka la Tanzania alipewa na rafiki yake, Uhuru Seleman ambaye kwa sasa yupo FC Lupopo ya DR Congo iliyomsajili akitokea timu ya daraja la kwanza ya Mbeya Kwanza.
“Uhuru nimecheza naye na alinieleza kila kitu kuhusu soka la Tanzania kabla sijaja na pia akaeleza kitu gani juu ya mashabiki wa soka wanachokitaka ndio maana imekuwa wepesi kwangu,” alisema.  Uhuru alithibitisha hilo kwa kusema ni kweli amekuwa na urafiki wa muda mrefu na Luis, hivyo alimweleza ugumu wa soka la Tanzania na vitu vya msingi ambavyo anapaswa kuvizingatia ili alizoee haraka.
“Nimecheza na Luis katika klabu mbili tofauti ni mtu ambaye tunafahamiana vizuri.”