Yanga kuondoka usiku wa manane leo kuifuata Township Rollers

Sunday August 18 2019

Mwanaspoti, Michezo, Tanzania, Yanga kuondoka, usiku wa manane, leo kuifuata Township Rollers,

 

By Bertha Ismail

Arusha. Kikosi cha Yanga kitaondoka mkoani Arusha leo usiku kuelekea Afrika Kusini na kuunganisha kwa basi kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Yanga sasa ipo uwanja ni ikicheza dhidi ya AFC Leopard ikiwa ni mchezo wake wa pili wa kirafiki katika kambi yake ya ukanda wa kaskazini baada ya mchezo wa awali kuchapwa 2-0 na Polisi Tanzania.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msola amesema baada ya mchezo huu watapanda ndege uwanja wa KIA saa saba usiku kupitia mjini Nairobi, Kenya wakielekea jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

"Tukifika Johannesburg tutatumia usafiri wa basi kwenda jijini Gaborone ambako tukaa huko hadi tutakapocheza mchezo wetu"

Dk Msola aliwataka wanachama na wapenzi wa Yanga kuiombea timu yao kheri huko wanakokwenda ili kufanikisha kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

"Uongozi na benchi zima la ufundi umefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha tunapata matokeo ikiwemo kutanguliza baadhi ya viongozi kuwatengenezea wachezaji mazingira mazuri nchini Botswana hivyo wanachama tunaomba ushirikiano wenu mkubwa hasa katika maombi."

Advertisement

Advertisement