Awesu aitanguliza Kagera Sugar

Friday November 8 2019

 

By Thomas Ng'itu

WINGA Awesu Awesu wa Kagera Sugar ameifungia bao la kuongoza timu yake katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya KMC unaondelea leo Ijumaa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Awesu alifunga goli hilo dakika 25 kwa mkwaju wa Penalti na kuifanya Kagera Sugar kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele  1-0.
Katika mchezo huo KMC inaongozwa na kocha wao msaidizi, Mrage Kabange baada ya kocha wao mkuu Jackson Mayanja kukosa vibali vya kufanyia kazi.
Kagera wanahitaji ushindi baada ya kupata sare katika mchezo wao uliopita dhidi ya Azam, huku KMC wakipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara Utd.
Matokeo mengine katika mechi za leo, Ndanda dhidi ya Yanga bado ni 0-0 mchezo unaopigwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Advertisement