Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xavi awekewa dau nono Saudi Arabia

XAVI Pict

Muktasari:

  • Xavi ambaye kwa sasa hana klabu tangu alipotimuliwa na Barca, Mei 2024 alikuwa na rekodi ya aina yake akiwa na kikosi hicho akishinda La Liga pamoja na Super Cup mwaka 2023.

BARCELONA, HISPANIA: KOCHA wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez ameripotiwa kupewa ofa nono na Al-ittihad ya Saudi Arabia jambo linaloweza kumshawishi kurejea tena kazini hivi karibuni.

Xavi ambaye kwa sasa hana klabu tangu alipotimuliwa na Barca, Mei 2024 alikuwa na rekodi ya aina yake akiwa na kikosi hicho akishinda La Liga pamoja na Super Cup mwaka 2023.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania ametafutwa na Ittihad ambayo inataka kocha mpya baada ya kumtimua Laurent Blanc.

Mfaransa huyo alitimuliwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi nne tu za Ligi Kuu Saudi Arabia akiiacha timu katika nafasi ya tatu.

XA 01

Al-Ittihad ilikuwa imeshinda mechi tatu kati ya nne ilizocheza, lakini bado mabosi hawakuridhika kwani timu ilikuwa nyuma ya  vinara wa ligi Al-Nassr.

Xavi si kocha pekee anayedaiwa kutafutwa na Al-Ittihad, pia Luciano Spalletti na Sergio Conceicao wanatajwa kuwa katika rada za timu hiyo.

Hata hivyo, licha ya pesa nyingi alizowekewa mezani na matajiri hao wa Saudia, ripoti zinadai Xavi anahitaji zaidi kujiunga na timu ya Ligi Kuu England hususani Manchester United ambayo muda wowote inaweza ikaachana na kocha wake Ruben Amorim kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na timu tangu kuanza kwa msimu huu.

XA 02

Xavi alianza kazi ya ukocha mwaka 2019 akiwa na Al-Sad ya Qatar ambayo aliisaidia kushinda Qatar Cup mara mbili na Qatar Stars League mwaka 2021.

Baadaye, mwaka huo huo 2021, alijiunga na Barcelona akichukua nafasi ya Ronald Koeman ambaye aliondoshwa kutokana na matokeo mabaya ya timu.