Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag amtaka Sterling

Muktasari:

  • Winga huyo wa Chelsea, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Arsenal  - amekuwa akifanya mazoezi kivyake baada ya kuelezwa na kocha Enzo Maresca kwamba hayupo kwenye mipango yake kwa ajili ya msimu uliopita.

MUNICH, UJERUMANI; CHAMA jipya la Erik ten Hag, Bayer Leverkusen linamfuatilia kwa karibu winga Raheem Sterling ikihitaji saini yake kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, imeelezwa.

Winga huyo wa Chelsea, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Arsenal  - amekuwa akifanya mazoezi kivyake baada ya kuelezwa na kocha Enzo Maresca kwamba hayupo kwenye mipango yake kwa ajili ya msimu uliopita.

Ripoti zinafichua kwamba Leverkusen ni miongoni mwa klabu zinazohitaji saini ya mkali huyo wa zamani wa kimataifa wa England.

Ten Hag, ambaye aliteuliwa kuwa kocha wa kikosi hicho cha Bundesliga, Mei mwaka huu, alijaribu kumsajili Sterling wakati alipokuwa akiinoa Manchester United.

Man United ilionyesha dhamira ya kumsajili Sterling kipindi alipokuwa akiwekwa benchi huko Chelsea, lakini dili hilo lilishindwa kutiki na mkali huyo alienda Arsenal.

Sterling aliitumikia kwa miaka saba timu mahasimu wa Man United, Manchester City na kwamba alikuwa tayari kwenda kucheza chini ya Ten Hag huko Old Trafford.

Lakini, sasa Ten Hag yupo Leverkusen ana anahitaji saini ya Sterling, ambaye timu yake ya Chelsea inahitaji Pauni 20 milioni tu kumfungulia mlango wa kutokea.

Juventus ni miamba mingine ya Ulaya inayohusishwa na staa huyo mwenye miaka 30.

Sterling amewekwa nje ya mipango ya Chelsea sambamba na wachezaji wengine, Joao Felix, Axel Disasi, Ben Chilwell na Djordje Petrovic, aliyetimkia Bournemouth.

Sterling bado ana mkataba wa miaka miwili, unaomshuhudia akilipwa mshahara wa Pauni 325,000 kwa wiki.