Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tchouameni aomba radhi baada ya ugomvi wa Valverde

Muktasari:

  • Tukio hilo lilihitaji wachezaji kadhaa pamoja na benchi la ufundi kuingilia kati kuzuia ugomvi usizidi, na pia lilisababisha adhabu ya kifedha ya Euro 500,000 iliyotolewa na klabu kwa wachezaji hao wawili kama hatua ya kinidhamu.

MADRID, HISPANIA: SIKU moja baada ya taarifa ya Federico Valverde kufuatia ugomvi kati yake na Aurélien Tchouameni huko Valdebebas, Hispania, kiungo huyo wa Ufaransa amevunja ukimya kupitia ujumbe mzito kwenye mitandao ya kijamii ambapo ameelezea kilichotokea kuwa “hakikubaliki” na kuonyesha masikitiko yake hadharani kuhusu picha ambayo yeye na mwenzake wameionyesha.

Tukio hilo lilihitaji wachezaji kadhaa pamoja na benchi la ufundi kuingilia kati kuzuia ugomvi usizidi, na pia lilisababisha adhabu ya kifedha ya Euro 500,000 iliyotolewa na klabu kwa wachezaji hao wawili kama hatua ya kinidhamu.

Katika taarifa yake, Tchouameni amesisitiza kuwa “kukata tamaa hakuwezi kuwa sababu ya kila kitu,” akiomba radhi kwa timu pamoja na mashabiki wa Real Madrid, na kuweka wazi kuwa kikosi kizima sasa kinapaswa kuelekeza nguvu zake kwenye mechi ya El Clasico dhidiya Barcelona kujaribu kuokoa matokeo mabaya ya msimu huu.

Jambo moja ambalo halijapita bila kuonekana ni kwamba, kama alivyofanya Valverde katika ujumbe wake juzi, Mfaransa huyo pia hakumtaja moja kwa moja mwenzake. Hakuna kati yao aliyetaka kumlaumu mwingine hadharani au kuelezea chanzo halisi cha ugomvi huo, mkakati ambao wote wameutumia kupunguza mvutano baada ya wiki ngumu ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya Real Madrid.

Mfaransa huyo hakusita kuelekeza nguvu kwenye El Clasico ili kupunguza uzito wa yaliyotokea akisema: “Huu sio wakati wa kutafuta nani alifanya nini, nani alisema nini au nani alikuwa sahihi au mwenye makosa... sasa ni wakati wa kuangalia mbele, na umakini wetu wote uko kwenye El Clasico na msimu uliobaki, ili kuirejesha klabu mahali inapostahili.”