Sterling, Chelsea ipo hivi

Sunday June 26 2022
rahim pic

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel, amewasiliana na Raheem Sterling, kabla ya kuweka ofa mezani Pauni 60 milioni, inayotakiwa na Manchester City, kwa mujibu wa ripoti.
Chelsea imepania kumsajili Sterling anayekipiga Manchester City, dirisha hili la majira ya kiangazi, huku taarifa zikiripoti Pep Guardiola yupo tayari kuachana na winga huyo.
Sterling, 27, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja wa kubaki Etihad, lakini Tuchel anataka kuongeza nguvu ili kuinasa saini ya winga huyo wa Kimataifa wa England, kwa mujibu wa taarifa.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano Chelsea chini ya Tuchel, imeendelea kupambana kuhakikisha Sterling anatua mitaa ya London, imeelezwa kuwa Tuchel anaamini watamshawishi winga huyo kuondoka Etihad.
Wakati hayo yakiendelea Tuchel ameshaanza mawasiliano na wawikilishi wa Sterling, pamoja na mchezaji mwenyewe, kabla ya kuweka Pauni 60 milioni mezani.
Taratibu za uhamisho wa Sterling zimeanza kimyakimya, huku Tuchel akitaka kufikia makubaliano binafsi ya mchezaji pamoja na wakala wake kwanza.
Aidha licha ya mkataba wa Sterling kufikia ukingoni Man City, winga huyo amefunga milango ya kujiunga na Chelsea dirisha hili, lakini kwanza anataka uhakika wa namba ya kudumu katika kikos cha kwanza.
Wakati huohuo Barcelona na Real Madrid wanafuatilia kwa makini, mwenendo wa uhamisho wa Sterling, kwani zimeanza kumtolea macho winga huyo aliyewahi kukipiga Liverpool.

Advertisement