Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yainyatia Chelsea kwa Simons

SPURS Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa RB Leipzig, Simons, 22, alikuwa anatarajiwa kuhamia Stamford Bridge baada ya jitihada za mazungumzo kufikia hatua nzuri.

LONDON, ENGLAND: KITENDO cha Chelsea  kuchelewa kukamilisha usajili wa kiungo wa RB Leipzig,  Xavi Simons kunaweza kufungua fursa kwa Tottenham kuingilia dili hilo na  kufanya uhamisho wa dakika za mwisho.

Nyota huyo wa RB Leipzig, Simons, 22, alikuwa anatarajiwa kuhamia Stamford Bridge baada ya jitihada za mazungumzo kufikia hatua nzuri.

Hata hivyo, Chelsea inaonakana kuchelewa  huku siku zikiwa zimebakia chache kabla ya dirisha la usajili kufunga Jumatatu ya wiki ijayo.

Tovuti ya The Sun, imefichua kwamba Chelsea inahitaji kwanza kuuza wachezaji zaidi ili kupata pesa za kufanyia usajili huo hali inayozua shaka ya dili hilo kufeli.

Tottenham imekuwa ikitafuta namba 10 mpya katika dirisha hili la majira ya kiangazi na ilijaribu kuwasajili  Morgan Gibbs-White na Eberechi Eze lakini wote iliwakosa..

Inaelezwa kwamba  Spurs inataka kuhamishia nguvu zao kwa Simons ambaye Spurs ipo tayari kumuuza kabla ya mwezi huu kumalizika.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anadaiwa kupendelea kuhamia Chelsea, lakini iwapo uhamisho huo hautatimia, huenda akalazimika kuzingatia dili hilo la Spurs.

Inadaiwa anahitaji mshahara mkubwa ili kutua timu yoyote ile inayomhitaji  wakati Leipzig ikihitaji Pauni 60 milioni kama ada yake ya uhamisho.

Mbali ya Simons, Spurs pia inataka kufanya jitihada za kuhakikisha inampata mchezaji wa Monaco, Maghnes Akliouche, 23, ambaye juzi (Jumatano) aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha taifa la Ufaransa.