Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford aambiwa aache starehe

Muktasari:

  • Rashford alianza msimu vibaya na jambo hilo limemfanya kulalamikiwa na mashabiki na kukosolewa na wachambuzi.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA, Marcus Rashford ameambiwa anapaswa kuachana na maisha yake ya starehe nje ya uwanja na kuwekeza akili ndani ya uwanja ili awe mchezaji bora kwenye kikosi cha Manchester United.

Rashford alianza msimu vibaya na jambo hilo limemfanya kulalamikiwa na mashabiki na kukosolewa na wachambuzi.

Fowadi huyo wa Man United kiwango chake kimeshuka tangu aliposaini mkataba mpya unaomshuhudia akilipwa Pauni 300,000 kwa wiki baada ya kufunga mabao 30 kwenye msimu wa 2022-23.

Msimu uliopita alifunga mabao manane katika mechi 43 alizocheza kwenye kikosi cha Man United, wakati msimu huu amefunga saba katika mechi 23.

Kushuka kwa kiwango kiasi hicho kumemfanya straika wa zamani wa Man United, Louis Saha kumtaka Rashford abadilike na kucheza kwa kiwango chake.

“Marcus ameanza kuonyesha uchu katika mchezo wa soka kama ilivyokuwa zamanai,” alisema Saha.

“Anahitaji kuonyesha huo uchu ili kuja kuwa mchezaji bora tena. Kama ataendelea kufanya mambo yake ya nje ya uwanja, madhara yake atayaona. Unaweza kufanya unachokitaka, unaweza kusafiri kwenda unakotaka, lakini siku zote kuna madhara makubwa. Unapokuwa na uchu na soka, hizo stresi haziwezi kuja.”

Saha alisema Rashford ambaye aliingia kwenye lawama nyingi baada ya kusafiri kwenda New York katika kipindi cha mapumziko ya mechi za kimataifa - na alikwenda kufanya starehe za nje ya uwanja wakati ana uwezo wa kumfanya afikie viwango vya kushinda Ballon d’Or.