Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho aitaka Real Madrid

Muktasari:

  • Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha Fenerbanhce ya Uturuki,  aliulizwa na kituo cha Cadena SER kama angekuwa tayari kufundisha tena Madrid ambayo hapo awali aliitumikia kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 akishinda mataji mbalimbali kama La Liga, Copa del Rey na Supercopa de España katika misimu yake mitatu.

MADRID, HISPANIA: MBWATUKAJI Jose Mourinho ameacha mlango wazi kuhusu kurejea tena Real Madrid, akisisitiza kuwa daima amekuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo.

Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha Fenerbanhce ya Uturuki,  aliulizwa na kituo cha Cadena SER kama angekuwa tayari kufundisha tena Madrid ambayo hapo awali aliitumikia kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 akishinda mataji mbalimbali kama La Liga, Copa del Rey na Supercopa de España katika misimu yake mitatu.

Kwa sasa mkataba wa kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti unamalizika Juni 2026 na Muitaliano huyo anadaiwa kuwa katika kuti kavu kutokana na matokeo mabaya ya timu.

“Daima nitaendelea kuwa shabiki mkubwa wa Real Madrid. Wana kocha bora duniani, rafiki yangu Carlo. Anafanya kazi vizuri sana,” alisema Mourinho.

“Mustakabali na uwezekano wa kwenda unategemea kile ambacho rais anataka, kama anataka kocha kijana mwenye maono makubwa kama Xabi Alonso au aendelee na mpango kuchukua makocha kama Carlo, mwenye uzoefu, au anaweza kuamua kuchukua kocha kutoka timu za vijana Raul na Alvaro Arbeloa. Inategemea.”

Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, ambaye alicheza chini ya Mourinho Bernabeu, ni miongoni mwa wale wanaotajwa kuwa wanaweza kupewa ajira hiyo na Mourinho anasisitiza kwamba yeyote atakayechaguliwa na Perez mara baada ya Carlo kuondoka atakuwa ni mbadala sahihi akiwamo na yeye.

“Florentino hajafanya uamuzi mbaya mara nyingi Madrid, nina uhakika mimi kama shabiki wa Madrid kuwa uamuzi wake ujao utakuwa sahihi,” alisema Mourinho matamo dhidi ya Athletic.