Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi vs Ronaldo muulize Casemiro

Muktasari:

  • Ni mjadala mkali kwa miongo miwili sasa kuhusu nani bora kati ya Ronaldo na Messi, licha ya Muargentina huyo baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022, alionekana kujiweka kwenye daraja lake, lakini mashabiki wa CR7 huwaambii kitu kuhusu mkali wao huyo ambaye ni supastaa wa kimataifa wa Ureno

LONDON, ENGLAND: KIUNGO Casemiro amesema Lionel Messi ni bora kumzidi Cristiano Ronaldo, licha ya Mbrazili huyo kucheza pamoja na CR7 kwenye timu mbili tofauti, Real Madrid na Manchester United.

Ni mjadala mkali kwa miongo miwili sasa kuhusu nani bora kati ya Ronaldo na Messi, licha ya Muargentina huyo baada ya kushinda Kombe la Dunia 2022, alionekana kujiweka kwenye daraja lake, lakini mashabiki wa CR7 huwaambii kitu kuhusu mkali wao huyo ambaye ni supastaa wa kimataifa wa Ureno.

Lakini, kauli ya Casemiro inaonekana kumaliza kila kitu, ambapo wengi walidhani kwa ukaribu wake kwa Ronaldo, basi angesema Mreno huyo kuwa ni bora, lakini badala yake bila kusitasita amesema Messi ni kiboko.

“Sikuwa naweza kabisa kumzuia peke yangu. Ilikuwa haiwezekani,” alisema Casemiro akimzungumzia Messi.

“Nilihitaji msaada wa watu wengine kama Toni Kroos, Luka Modric, Sergio Ramos...lakini peke yangu, ilikuwa haiwezekani. Alikuwa hazuiliki.”

Casemiro alisifu viwango vya wachezaji hao wawili kwa kudumu kwenye ubora kwa muda mrefu, alisema Messi ni mwanasoka bora kwenye historia ya soka, lakini Ronaldo naye ni mchezaji mwingine matata. Ronaldo na Messi wanaripotiwa kubadilika kulingana na matakwa ya soka linavyohitaji na ndiyo maana wapo juu kwa muda wote.

Wawili hao kwa pamoja wameshinda Ballon d’Or, Messi mara nane na Ronaldo tano na walichuana jino kwa jino kwenye La Liga kabla ya kila mmoja kwenda na njia zake.