Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi afunguka ushindani na CR7

Muktasari:

  • Kwa sasa wakicheza Inter Miami nchini Marekani na Al-Nassr ya Saudi Arabia mtawalia, wawili hao waliwahi kupambana katika kiwango cha juu zaidi wakizichezea Barcelona na Real Madrid. Pia walikuwa na ushindani binafsi huku wakibadilishana ushindi wa Ballon d'Or kwa miaka kadhaa. Messi ana Ballon d'Or nane huku Ronaldo akiwa nazo tano.

MIAMI, MAREKANI: SUPATAA wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amezungumza kuhusu "ushindani bora wa kimchezo" kati yake na nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo uliowashuhudia wawili hao waliotajwa kuwa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea wakikabiliana mara nyingi katika maisha ya soka.

Kwa sasa wakicheza Inter Miami nchini Marekani na Al-Nassr ya Saudi Arabia mtawalia, wawili hao waliwahi kupambana katika kiwango cha juu zaidi wakizichezea Barcelona na Real Madrid. Pia walikuwa na ushindani binafsi huku wakibadilishana ushindi wa Ballon d'Or kwa miaka kadhaa. Messi ana Ballon d'Or nane huku Ronaldo akiwa nazo tano.

“Kilichotokea kilikuwa ushindani mzuri wa kimichezo,” Messi ameiambia Pollo Alvarez kuelekea fainali za Kombe la Dunia pamoja na El Clasico ya wikendi hii kati ya timu zao za zamani za Hispania.

“Ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa soka. Mimi nilikuwa Barcelona na yeye alikuwa Real Madrid, na tulikuwa tunashindania kila kitu kama timu na binafsi, hivyo watu walikuwa wakitulinganisha kila wakati. Lakini uhusiano wetu ulikuwa mzuri na wa heshima kila wakati, na kila kilichotokea kilikuwa cha kimichezo. Hakukuwa na mambo binafsi.

“Hatukuwa tukikutana mara nyingi isipokuwa kwenye mechi au hafla za tuzo, na siku zote tulikuwa na mahusiano mazuri. Sasa tuko katika hatua tofauti za maisha yetu, lakini kilichotokea ulikuwa ushindani mzuri wa kimichezo.”

Timu hizo mbili zitachuana wikendi hii katika El Clasico huku Lamine Yamal ambaye hatacheza akiendelea kuvaa jezi namba 10 Barcelona iliyowahi kuvaliwa na Messi.

Na hilo ni jambo ambalo Messi amezungumzia katika tukio la Adidas baada ya kutolewa kwa tangazo rasmi la Kombe la Dunia ambalo yeye na Yamal wameonekana pamoja.

“Kuna kizazi kipya cha wanasoka wazuri sana na wenye miaka mingi mbele. Lakini kama ningetakiwa kuchagua mmoja kutokana na umri wake, kile alichofanya hadi sasa na mustakabali wake, basi ningemchagua Lamine. Bila shaka yoyote, kwangu yeye ndiye bora zaidi," alisema Messi.

Yamal na Messi wanaweza kukutana uso kwa uso msimu huu katika Kombe la Dunia huku Argentina na Hispania zikiwa miongoni mwa timu zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa. Wakati Messi aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2022, Yamal aliisaidia Hispania kushinda Euro miaka miwili baadaye.