Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wanne hali mbaya Man United

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao wanne watatakiwa kufanya mazoezi kivyao na wasichanganyane na wachezaji wa kikosi cha kwanza wakati watakaporejea England wakitokea Marekani wiki ijayo.

MANCHESTER, ENGLAND: MASTAA wa Manchester United, Alejandro Garnacho, Antony, Jadon Sancho na Tyrell Malacia bado wapo bayana baada ya kutakiwa kutowasogelea kabisa mastaa wengine wa kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Old Trafford.

Wachezaji hao wanne watatakiwa kufanya mazoezi kivyao na wasichanganyane na wachezaji wa kikosi cha kwanza wakati watakaporejea England wakitokea Marekani wiki ijayo.

Wachezaji hao waliopachikwa jina la ‘Bomb Squad’ wameruhusiwa kuendelea kufanya mazoezi kwenye viwanja vya Carrington, lakini wamepangiwa ratiba tofauti kabisa na ile ya wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Ripoti zinadai kwamba awali walitakiwa wakafanye mazoezi na kikosi cha umri chini ya miaka 21, lakini kwa hofu ya kufunguliwa mashtaka, imeamua kuwaruhusu wafanye mazoezi kivyao, wakipewa projekti yao tofauti.

Chanzo kilifichua: “Watafanya mazoezi kama kundi, lakini kwa ratiba tofauti kabisa na kikosi cha kwanza. Kikosi cha kwanza kitafanya mazoezi asubuhi, wao watafanya mchana.”

Na kocha mkuu wa miamba hiyo ya Old Trafford, Ruben Amorim amewaambia watafute timu nyingine za kwenda kuchezea, kwa sababu hawapo kwenye mipango yake kwa ajili ya msimu ujao.

Man United chini ya Amorim ilimaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, hivyo kocha huyo Mreno anajaribu kuondoa wachezaji wote anaodhani hawapo kwenye mipango yake ili kuja kivingine.

Man United itacheza mechi ya mwisho ya pre-season huko Marekani kwa kukipiga na Everton.