Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki wasusia gemu ya Chelsea

MASHABIKI Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyoanza saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashabiki  saa 9:00 alasiri muda wa kazi Jumatatu kwa saa za huko Atlanta, ulifanyika kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz.

ATLANTA, MAREKANI: CHELSEA imetupa kete ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani dhidi ya Los Angeles FC usiku wa Jumatatu ikicheza kwenye uwanja wenye siti tupu kibao huko Atlanta.

Mechi hiyo iliyoanza saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashabiki  saa 9:00 alasiri muda wa kazi Jumatatu kwa saa za huko Atlanta, ulifanyika kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz.

Mashabiki waliohudhuria mechi hiyo, ambapo Chelsea ilishinda 2-0 walikuwa 22,137, wakati uwezo wa uwanja ni kuingiza mashabiki 71,000 - hivyo siti nyingi za uwanja zilibaki wazi, huku jukwaa la juu kabisa likifungwa.

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, alisema: “Nadhani mazingira yalishangaza sana, uwanja ulikuwa mtupu, haukujaa. Sisi ni profesheno, yatupasa kukabiliana na hali ilivyo, mazingira. Lazima, tuzoee unapocheza kwenye uwanja uliojaa au unapocheza usiojaa.”

Katika mechi hiyo ya Chelsea, tiketi ya bei rahisi kabisa ilikuwa Pauni 37, ambayo ni karibu Sh130,000 kwa pesa ya Kitanzania. Lakini, wakati mechi hiyo inachezwa, tiketi zilikuwa bado zinauzwa mtandaoni kwa Pauni 26 - ambayo ni zaidi ya Sh 90,000 ya Kitanzania.

Los Angeles ipo umbali wa zaidi maili 2,000 kutoka Atlanta, upande wa kusini mwa Marekani. LAFC iliingia kwenye mechi hiyo kuchukua nafasi ya Leon, ikitajwa kuwa huenda ikawa sababu nyingine ya kushindwa kuvutia mashabiki wengi katika mechi hiyo.