Mane ndani ya uzi wa Bayern

Thursday June 23 2022
mane pic

MUNICH, UJERUMANI. SADIO Mane ametambulishwa rasmi na miamba ya Bundesliga baada ya kukamilishan uhamisho wake uliyogharibu kitita cha Pauni 35 milioni akitokea Liverpool, alipokuwa akikipiga kwa muda wa miaka sita.
Mane amesaini mkataba wa kukipiga Bayern Munich hadi mwaka 2025, na atakinukisha Bundesliga msimu mpya utakapoanza.
Aidha Mane amesema licha ya kijiunga na miamba hiyo, ataendelea kuisapoti Liverpool katika mashindano yote itakayoshiriki.
Fowadi aliweka wazi anataka kuondoka Liverpool na kutafuta changamoto upande mwingine, baada ya fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya.
Hadi anaondoka Anfield, Mane amefunga mabao 120 katika mechi 269 alizocheza mashindano yote, na kuisainia Liverpool mataji kadhaa kama Ligi Mabingwa Ulaya, FA, Caraba na ligi.

Advertisement