Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City, Man United nyota kibao wamesepa

WAMESEPA Pict

Muktasari:

  • Yamepita madirisha matatu ya usajili tangu miamba hiyo ilipokutana kwenye fainali ya Kombe la FA mwaka 2024 na Man United iliichapoa Man City 2-1 na kunyakua taji hilo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City na Manchester United zitamenyana jino kwa jino Jumapili katika mechi ya 197 ya Manchester Derby.

Yamepita madirisha matatu ya usajili tangu miamba hiyo ilipokutana kwenye fainali ya Kombe la FA mwaka 2024 na Man United iliichapoa Man City 2-1 na kunyakua taji hilo.

Lakini, tangu wakati huo kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vikosi vyote vilivyokutana uwanjani Wembley katika mchezo wa fainali.

Man United ina wachezaji saba tu waliobaki kwenye kikosi hicho, mabadiliko ambayo pia yamekuwa makubwa huko kwa miamba ya Etihad.

Kuna wachezaji 21 tu kutoka kwenye timu zote kati ya 40 wameachwa na timu hizo tangu kikosi kile kilichokutana Wembley.

Kwa kuanzia kwenye kikosi cha Man United, kuna wachezaji 13 kati ya 20 wameondoka, akiwamo kocha Erik ten Hag, huku kipa Andre Onana, naye akiachana na timu hiyo Alhamisi iliyopita alipokwenda kujiunga Trabzonspor.

Mabeki Aaron Wan-Bissaka na Raphael Varane waliokuwapo kwenye kikosi hicho cha ubingwa, nao wameondoka.

Wachezaji wa Man United waliondoka kikosini tangu wakati huo wa fainali ya Kombe la Ligi ni Onana, Wan-Bissaka, Varane, Sofyan Amrabat, Alejandro Garnacho, Marcus Rashford, Scott McTominay, Victor Lindelof, Jonny Evans, Willy Kambwala, Christian Eriksen, Rasmus Hojlund na Antony. Kwenye kikosi cha Man City, waliondoka ni Kyle Walker, Kevin De Bruyne, Scott Carson, Manuel Akanji na Jack Grealish, Julian Alvarez.