Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Barca kichwa kinauma

Muktasari:

  • Kipa Joan Garcia amepata majeraha akiwa mazoezini, pia winga wao kutoka Brazil, Raphinha atakaa nje kwa wiki tatu kutokana na jeraha la msuli wa paja, na hivyo wote kukosa mechi za michuano ya ndani na kimataifa.

BARCELONA, HISPANIA: KOCHA wa Barcelona, Hansi Flick anakabiliwa na kibarua kigumu cha uchaguzi wa kikosi kabla ya mtanange muhimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain.

Kipa Joan Garcia amepata majeraha akiwa mazoezini, pia winga wao kutoka Brazil, Raphinha atakaa nje kwa wiki tatu kutokana na jeraha la msuli wa paja, na hivyo wote kukosa mechi za michuano ya ndani na kimataifa.

Wababe hao wamethibitisha kuwa Garcia alipata jeraha katika mazoezi ya Ijumaa, huku Raphinha akikumbwa na tatizo la msuli wa paja la kulia litakalomweka nje kwa karibu wiki tatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari, Raphinha ataukosa mchezo wa leo, Jumapili wa La Liga dhidi ya Real Sociedad, mechi inayofuata dhidi ya Sevilla, pamoja na mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG.

Marcus Rashford, ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu hivi karibuni, anatarajiwa kuziba nafasi yake upande wa kulia.

Hata hivyo, bado kocha Flick kichwa kinauma kutokana na jeraha la Garcia,  ambaye ni kipa wake namba moja na alimhitaji sana kuelekea mechi zijazo muhimu.

Kipa huyo alipata jeraha wakati wa mazoezi ya Ijumaa, asubuhi na ripoti ya madaktari inaeleza amepata mpasuko wa ndani katika goti lake la kushoto, hivyo  ilibidi afanyiwe upasuaji mdogo (arthroscopic) chini ya daktari Joan Carles Monllau na atakuwa nje kwa wiki nne hadi sita.

Hali hii inamlazimisha Flick kumtegemea Wojciech Szczesny, kipa mkongwe wa Kimataifa wa Poland, ambaye ana uzoefu wa michezo mikubwa lakini kuna wasiwasi kwa sababu ya umri wake na amekuwa hapati sana nafasi kikosini.