Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kivumbi kinaendelea tena wikiendi hii

KIVUMBI Pict

Muktasari:

  • Kasheshe litaanzia Etihad mchana, ambapo Manchester City itakuwa nyumbani kukabiliana na Tottenham Hotspur. Kipute hicho kitavuta hisia za wengi kuona itakavyokuwaje.

LONDON, ENGLAND: JOTO la Ligi Kuu England litapanda tena wikiendi hii ambapo timu zitarusha kete za pili kwenye mchakamchaka wa kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Kasheshe litaanzia Etihad mchana, ambapo Manchester City itakuwa nyumbani kukabiliana na Tottenham Hotspur. Kipute hicho kitavuta hisia za wengi kuona itakavyokuwaje.

Baada ya mechi hiyo, kutakuwa mechi tatu zitakazofanyika muda mmoja, Jumamosi hii, ambapo Bournemouth itakuwa nyumbani kuikaribisha Wolves, huku Brentford itaulizana maswali magumu na Aston Villa, wakati Burnley itakuwa na shughuli pevu mbele ya Sunderland, katika moja ya mechi zinazotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Mechi ya mwisho kwa Jumamosi itakuwa huko Emirates, ambapo Arsenal itarusha kete yake ya kwanza nyumbani kwenye Ligi Kuu England itakapokipiga na Leeds United. Kwenye mechi hiyo, macho ya wengi yatakuwa kwa straika Viktor Gyokeres kama ataanza kufungua akaunti yake ya mabao kwenye Ligi Kuu England.

Kesho, Jumapili kwenye Ligi Kuu England kutakuwa na mechi tatu tu, ambapo Everton itakuwa nyumbani kucheza na Brighton, huku Crystal Palace ikikipiga na Nottingham Forest, wakati Manchester United iliyochapwa kwenye mechi ya kwanza ilipocheza nyumbani Old Trafford mbele ya Arsenal, itakuwa ugenini kukipiga na Fulham.

Jumatatu kutakuwa na mechi moja tu, ambapo Newcastle United itakuwa nyumbani St James’ Park kukabiliana na Liverpool, ambayo imekuwa ikimtia kizunguzungu straika wao, Alexander Isak kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, wakitaka huduma yake.