Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane aipa ubingwa wa UEFA PSG

Muktasari:

  • Arsenal ilitinga fainali hiyo baada ya kuichapa Atletico Madrid bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali ya pili baada ya kutoka sare ya kwanza huku PSG wakiondoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 6-5 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Munich.

MUNICH, UJERUMANI: MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Harry Kane amesema Paris Saint-Germain ina nafasi kubwa ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal na anaona itakuwa mechi yenye ushindani mkubwa.

Arsenal ilitinga fainali hiyo baada ya kuichapa Atletico Madrid bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali ya pili baada ya kutoka sare ya kwanza huku PSG wakiondoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 6-5 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Munich.

Kane alisema anaamini timu hizo mbili zina ubora mkubwa tofauti na namna zinavyocheza, jambo litakaloifanya fainali hiyo kuwa na mvuto.

“Nafikiri mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa sana. Ni timu mbili tofauti kwa mtindo wa uchezaji lakini zote zina nguvu kubwa,” alisema Kane.

Straika huyo aliendelea kueleza PSG wanaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi kutokana na uzoefu wao kwenye mashindano hayo.

“PSG kama mabingwa watetezi wanaweza kupewa nafasi kubwa kidogo, lakini kwa jumla naamini itakuwa fainali ngumu na ya wazi kwa timu yoyote kushinda,” alisema Kane.

Kwa upande wake, kocha wa PSG, Luis Enrique alisema Arsenal inastahili kabisa kucheza fainali hiyo kutokana na kiwango ilichoonyesha msimu mzima.

“Arsenal imekuwa bora sana msimu huu na ilistahili kufika fainali. Lakini hii ni fainali, kila timu inataka kushinda,” alisema Enrique.

Kocha huyo wa PSG aliongeza timu yake inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuendelea kuweka historia mpya ndani ya klabu hiyo ya Paris.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa  kati ya Arsenal na PSG inatarajiwa kupigwa Mei 30 mjini Budapest huku Arsenal wakisaka ubingwa wao wa kwanza wa Ulaya na PSG wakitaka kutetea taji lao kwa mara nyingine tena.