James Rodriguez atafuta njia ya kurudi Ulaya
Muktasari:
- Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ame-onyesha kwamba bado anaweza kucheza soka la kiwango cha juu baada ya kuupiga mwingi kwenye Copa America akiiwezesha timu yake ya taifa kumaliza ya pili katika michuano hiyo ya kimataifa.
SAO PAULO, BRAZIL: JAMES Rodriguez ameripotiwa kujipanga kuondoka Sao Paulo akisaka kurejea katika soka la Ulaya baada ya kufanya mambo ma-kubwa akiwa na timu ya taifa ya Colombia kwenye Copa America.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ame-onyesha kwamba bado anaweza kucheza soka la kiwango cha juu baada ya kuupiga mwingi kwenye Copa America akiiwezesha timu yake ya taifa kumaliza ya pili katika michuano hiyo ya kimataifa.
Rodriguez pia aliweka rekodi mpya ya Copa America kwa kutoa asisti sita zilizomsaidia kushinda tuzo Mchezaji Bora wa Michuano hiyo.
Baada ya kung’aa na Colombia, kwa mujibu wa mwandishi wa habari Garcia Grova, Rodri-guez anajiandaa kuvunja mkataba wake na Sao Paulo na kwenda kujaribu bahati Ulaya katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi.
Kiwango chake katika mechi za siku za hivi ka-ribuni kimethibitisha kwamba bado ana uwe-zo mkubwa wa kuwasha moto na inatarajiwa klabu nyingi za Ulaya zitavutiwa kuipata saini yake
Mkali wa habari wa usajili, Fabrizio Romano aliongeza kwamba Rodriguez "atapenda" ku-rejea Ulaya.
Miezi kadhaa nyuma, Rodriguez alidokeza kuhusu uwezekano wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Everton.
Maisha ya soka ya Rodriguez yamejaa majina makubwa ya klabu ambazo amewahi kuzitu-mikia Ulaya, ikiwamo Real Madrid, Bayern Munich, na Everton.